Irmã Maria Alice Schimit

Utambuzi wa uwepo wa Yesu ndani ya maisha yetu, ukifanyika kila mara ni alama ya ushindi.

Kwa kupitia Sheria ya kipapa, Shirika letu limetajirishwa kwa kupewa sifa ya kuwa la “kimisionari” kama hadhi yake.  Utendaji na ushiriki wetu katika kueneza Injili umedhihirika kuwa ni jambo la msingi kupitia uwepo wetu kwa Kanisa na kwa dunia. Wengi wa masista wetu wamejikita katika utoaji wa huduma kwenye misioni mbali na nchi zao walikozaliwa. Yote yakiongozwa na roho ya kimisionari, wameitikia – Ndio – kwa mwaliko wa Bwana wa “kuingia kabisa ndani ya kina cha maji baharini”, kwa nia ya kuchangia kuiitangaza Injili na kumfanya Yesu atambulike kwa wote. Baada ya kufanya kazi kwa bidii kwa miaka mingi kwa shule ya vichekechea na ya awali huko San Paolo na Parana, bila kutarajia nilipata ombi kutoka kwa mama Mkuu: <>. Haikuwa rahisi kwangu kuacha yote ili nitoe jibu langu la – Ndio – , toka siku ya kupata ombi hilo, kuna swali ambalo nilijiuliza daima: ‘Yesu angefanya nini angekewa ndiye mimi?’ Lakini…ili yote haya yaweze kuwa na maana halisi, huku kila jambo likiwa tayari limeamuliwa na kukamilika, ikawa siku moja kabla ya kuondoka kuanza safari, bila kutarajia mama yangu alipata ugonjwa wa kuanguka ghafla. Niliahirisha safari kwa muda na baada ya kumhudumia kwa siku kadhaa hadi afya yake ikawa na unafuu, kwa njia ya wosia wa Wakubwa wangu na kutiwa moyo na kaka zangu, niliondoka kuelekea Guatemala. Nimemwacha Mama ambaye hakuwa na uwezo tena wa kutembea, wa kula, wa kuongea, sijui…leo, sitaweza kama sitaweza kuwashukuru wakubwa wangu kwa uelewa wao, kaka zangu kwa kunitia moyo. Nilipofika huko, nilimwomba Bikira Maria aweze kumponya mamangu ili niweza kutoa ushuhuda kwa wote kuwa kupona kabisa kwa mama yangu ni miugiza kwani sasa amerudia hali yake ya kawaida, licha ya kuwa bado mara kwa mara uwezo wa kumbukumbu unampotea.

Licha ya kupata kwake nafuu kwa haraka, lilitokea jambu jingine jipya: yeye anaongea nami kupitia mtandao wa mawasiliano wa kompiuta unaojulikana kama Skype; ntasema nini juu ya mama yangu, mwanamke mpole na mnyenyekevu anayaeongea nami kupitia kompiuta? Mtawa mwenzangu mzoefu shughuli za kimisionari aliniambia: “kupona kwa mama yako ni muujiza unaotokana na – Ndio – yako. Nami baada ya hapo nimeanza kuzoea kwa haraka. Nashiriki katika utume parokiani na kutoa huduma kwa watu ambao ni wahitaji wa kweli na ninajihusisha na huduma kwa wasichana wanaopanga kwenye bweni la EIEstor, linalosimamiwa na jimbo.

Baada ya miezi kadhaa ya uwepo wangu hapa, niliweza kuonja furaha ya miaka yangu 25 ya utawa. Misa takatifu ni wakati wa muungano wa kindugu, wa kukaa wote pamoja, hata kusherehekea na kuendelea kwenye nyumba yetu nyingine, huko Quirigua. Wanafamilia na masista lichaa ya umbali wao, bado niliweza kujisikia kuwa karibu na wakati wa adhimisho la Misa niliweza kusali hivi: – “Leo, namshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha na ya wito, na kwa Shirika la Masista Wamisionari wa Mioyo Mitakatifu, kwa kunipokea; kwa nia ya familia yangu na kwa wote wale walionitia moyo katika safari ya kuitikia wito wa Mungu na kunisaidia kufikia hapa nilipo: kwa ajili ya baba yangu na marafiki zangu ambao tayari wametangulia mbele ya Mungu, natoa shukrani yangu isiyo na mwisho kwao wote. Nyote hapa, ambapo siku hii ya leo pamoja nami tumeinua mioyo yetu kwa Mungu kwa tendo hili la shukrani kwa ajili ya miaka yangu 25 ya maisha ya kitawa, tumshukuru Mungu. Napenda kama Yesu kudumu daima katika kutenda yaliyo mema. Mniombee ili niweze kudumu katika utume na kuwa mwaminifu na kutenda yote daima kwa faida ya ndugu zangu. Kwa vijana wote mliopo hapa, nawageukia kuwaalika kumfuasa Yesu, kwa ajili ya kuyatolea maisha yenu yote kwa njia ya kueneza Injili, ili kuufanya ujulikane kwa wote ukubwa wa upendo wa Moyo wake na kutolea, kwa ajili ya nchi ya Guatemala, uso mpya: ule wa amani, wa kuheshimiana na wa kuonja kwa pamoja kidogo kilichopo, kupunguza ule uhasama ambao kila mara unasababisha maangamizi kati ya ndugu na ndugu, rafiki na rafiki. Njoni na kumtambua Yesu na sote pamoja tutapata nguvu itayobadilisha taifa letu kuwa familia mmoja. Katika kumfuasa Yesu huwezi kamwe kupoteza chochote; unakuwa mwema zaidi, mwenye ubinadamu zaidi, mwenye undugu zaidi. <>. Asanteni.

Questo sito o gli strumenti terzi da questo utilizzati si avvalgono di cookie necessari al funzionamento ed utili alle finalità illustrate nella cookie policy. Se vuoi saperne di più consulta la nostra Informativa. Cliccando su Approvo acconsenti all’uso dei cookie. Maggiori Info | Approvo