Misioni

Mungu, Baba anayetupenda anaongea nasi na wote twaunganishwa na Neno lake. Kila moja wetu anapaswa kujitoa kwa dhati kwa kumsikiliza. Kulisikia Neno la Mungu kwatusaidia kufika mahali panapofaa kuyapa umana maisha yetu.


 TENDO LA KUITIKIA


Wito wa Yesu: «Njooni nanyi mtaona» (Jn . 1,46), Ni wito ulio mbele ya vijana wengi wenye mwamko na wanaojihusisha kwa sasa katika matendo mema, kwa lengo la kuwasaidia wenye shida. Wito wa Yesu «Kauze yote na kisha nifuate» ni mwaliko kwa vijana wote wanaotafuta mwelekeo halisi wa maisha, unaodai mwitikio dhahiri bila kusitasita, na hivyo kuwezesha kubaki na Yesu na kupokea utume kwa ajili ya ndugu zako.

Tendo la kutumwa kutangaza Habari Njema ya Wokovu kwa njia ya umisionari latudai usikivu wa hali ya juu na wa kudumu, ili tuweze kuishi kile tunachokisikia na kugawa kile tunachokiishi. Kwenu vijana, toka kwa moyo mkunjufu na wenye huruma twatolea utayari wetu kwani twapenda uweze kutambua wito wako na kuweza  kusema’mimi hapa nitume’ ambao ndio wito Yesu anawaitia.

  • Makutano ya kiwito
  • Mawasaliano
  • Kujituma mwenyewe
  • Uzoefu katika jumuia zetu

 MALEZI


Wamisionari wa Mioyo Mitakatifu ya Yesu na Maria wameitwa kudumu katika kupokea malezi ya kina, toka kwa wenzao walio na umri mkubwa hadi wa ngazi mbali mbali hadi wale walio katika umri wa ujana ambao bado wako katika hatua za awali za kuingizwa kwenye wito wa Mungu.

Upostulanti hudumu kwa muda wa mwaka mmoja, ingawa unaweza kukadiriwa kadiri ya mahitaji ya kila mkandidati; lengo lake la msingi ni kutoa malezi ya ukomavu wa kiutu na kikristu, hadi yule aliyeitwa aweze kuchagua kwa uhuru wote maisha ya wakfu katika familia yetu ya kitawa kama dira ya kila mtu na kuweka mbele mambo ya msingi kadiri ya mpango wa Mungu.

Unovisi hudumu kwa muda wa miaka miwili muda ambapo kijana atasaidiwa kufanya mazoezi ya dhati ya sala na usikivu wa Neno la Mungu, pia moyo wa kindugu na kitume; mambo ya msingi na yanayojulikana ya maisha yetu ya umisionari, yakitimizwa pamoja na Yesu kwa muungano wa ndani ambao toka kwayo huchomoza kila shughuli ya kitume na hivyo kumpa uwezo wa kumwezesha kuuishi utawa.

Ujunirato hudumu kwa muda wa miaka mitano, isipokuwa kwa sababu ya msingi unaweza kuongezwa; wenyewe una lengo la kuimarisha kwa kuunganisha hatua kwa hatua malezi yote ya awali, hadi kufikia hatua ya kulandana na sura ya mtu shupavu na mwenye maamuzi katika kutimiza kile ambacho Bwana na Kanisa vyategemea toka kwake; kumtumikia Mungu na ndugu zetu kadiri ya matakwa na mpango wa Shirika.

Malezi Endelevu yanadumu kwa maisha yote, kwani yeyote aliyejiweka wafu hawezi kutamka kabisa kuwa amefikia kikomo cha kumuunda yule mtu mpya ambaye anamtafuta ndani mwake, ili kwa kila hatua ya maisha,  aweze pata hisia zile zile za Kristo. Malezi ya mwanzo lazima yatokane na yaunganike na yale endelevu, ili yaweze kumuundia mtu utayari wa kujitoa kwa malezi ya kila siku ya maisha.


 UTUME


Tangu awali Shirika letu lilipoanzishwa limekuwa likijihusisha katika maeneo mbali mbali ya utume maalumu ambao yanahusishwa na mwanzo wake na ambao yanaendelea bado; mafundisho ya katekisimu, kuwasaidia watu katika kukua kwao kumtambua Kristo, ushawishi wa dhamiri za watu katika kutambua umuhimu na thamani za Masakramenti, hasa kumunyo ya kwanza, ili kukuza kwa mioyo ya walio wadogo Upendo mkubwa kwa Yesu kama mwitikio kwake wanaoudhihirisha  katika kukutana kwao.

Namns hii ya mwonekano wetu ni sehemu inayotuunganishi na Karama yetu ambapo twafuata mfano wa Kristo katika kutekeleza utume wake wa kutangaza ukombozi kwa kujihusisha na huduma za Utawala ndani ya kazi za kichungaji, hivyo kutekeleza upendo wa kindugu kwa matendo, kadiri ya utaratibu wa Shirika unaotambulika kama jambo la msingi ndani ya uwepo wa Kanisa kwa ajili ya Kanisa. Twatambua kwa umakini wa pekee kuenea kwa ibada za uchaji na kujiweka wakfu kwa familia kwa Mioyo ya Yesu na Maria. Ibada hizo zaweza kutoa ushuhuda wa kweli wa maisha yao ya kikristu, kupata njia ya kujitakatifuza katika hali zao za uanafamilia na kufanikisha kadiri ya uwezo wao ushawishi wa kujiweka karibu na Mioyo ya Yesu na Maria.

Tumezaliwa kwa njia ya karama ndani ya Kanisa ili kudhihirisha wazi unyenyekevu na upendo wa Moyo wa Yesu mbele ya binadamu wote, hasa kwa wale wanaohitaji. Kama ‘wamisionari’ twahisi kuwa upeo wa ushiriki wetu katika uenezaji wa Injili umekuwa kama sehemu mojawapo ya msingi ya uwepo wetu katika Kanisa na kwa ulimwengu, kwa njia za kazi za matendo ya huruma ambazo watu wa nyakati zetu wanazitegemea.


 KARAMA NA MAISHA YA KIROHO


Tangu mwanzo wa Shirika letu, Karama ya Kiroho na Karama ya kitume, vimedhihirishwa na moyo wa kujitolea kabisa wa kila mwanashrika katika kueneza utawala wa Mungu kwa kila ndugu kwa njia ya kuutangaza upendo wa Baba, kwa njia ya kuwaalika waweze kuishi ndani ya wokovu wa Mwana wa Mungu huku wakiwa wanaongozwa na busara itokayo kwa Roho Mtakatifu. Wamisionari wa Mioyo Mitakatifu wanaimarisha na kuendeleza kwa maisha yote malezi ya kina, ili mwishowe waweze kuufikia utakatifu unaodaiwa kwa kila mbatizwa na kwa kujiweka kwao wakfu kwa maisha ya kitawa. Machimbuko ambayo kila moja anayaheshimu ni Biblia Takatifu, Tabanaklo, vitabu vya kufaa, vitu  ambavyo vyatuwezesha kupata uelewa wa sadaka ambayo Yesu na Maria waliitolea ndani ya maisha yao kwa Mungu Baba.

Kila moja anapaswa kuidhihirisha hio sadaka kwa furaha akiishi maisha ya kujiweka wakfu akiangazwa na mwanga wa Moyo wa Yesu na kujilinganisha na mfano wa maisha ya moyo wa Maria ambapo kwa kila mmoja ni mfano wa kuigwa wa maisha katika kutimiza lengo la ufuasi wa Yesu.

Kila mmoja wetu katika mwenendo wake wa kibinadamu na kiroho anatamani: “kuuishi ufuasi wa Moyo wa Yesu, ndani ya mwanga wa Moyo wa Maria, kwa lengo la kutoa huduma kwa ndugu zetu walio maskini na wanaoteseka“, ikiwa ni alama ya ndani na yenye nguvu ya kujiweka wakfu kwa dhati kwa kuitikia wito wetu kikamilifu, kwa kuwajibika na kwa juhudi binafsi tukiwa tumeungana na Kristo ambaye daima anatualika tuweze kujifunza kwake: upole, unyenyekevu, utumishi, upendo kwa Mungu na kwa ndugu zetu na kwa Maria mtakatifu sana kama mfano wa imani, wa utayari na usafi wa akili na moyo.


 USHUHUDA


» Irmã Maria Alice Schimit

» Sr Maria Concetta Porto