Waanzilishi wa Shirika

Madre Rosa Rosato

Mama Rosa Rosato alizaliwa huko Lanciano mnamo tarehe 27 Julai 1858, wazazi wake ni Salvatore na Giovanna Pasquin, waliokuwa wakulima waliomiliki nyumba na ardhi. Ni mtoto wa tatu kati ya watoto kumi. Alijiunga kikamilifu na muungano wa Chama cha wito hapo tarehe 26 Disemba 1984.

Madre Rosa Rosato

Ndani ya familia mpya ya kitawa, iliyoanzishwa Roma, yeye ndiye akawa Mama Mkuu wa kwanza na mwaka 1911 palifanyika Mkutano Mkuu wa Shirika wa kwanza, na ndipo wakubwa wa Kanisa walitambua toka kwake uadilifu wa hali ya juu na unyenyekevu, upole na uwajibikaji na hivyo wakamteua kuwa Mama mkuu wa kwanza wa Shirika. Katika nyakati za utulivu na mazingira`magumu, yeye aliliongoza Shirika kwa busara kubwa iliyochota nguvu ndani ya tabanaklo na bila kujali magumu. Katika mazingiza mengi ‘ya uanzilishaji wa Shirika’ yeye aliweza kudhihirisha uwezo wa malezi ya mfano, maisha ya ndani ya kiroho na juhudi zisizo na kikomo katika shughuli muhimu za Shirika. Uwepo na utayari wake ulijitokeza wakati wote kwa kila mmoja na kwa kila hali, akiishi maisha ya uchaji wa ndani. Kwa mabadiliko ya shughuli za wakati huo, kwa kufuatilia aliyokabidhiwa, alipoachwa huru kutoka shughuli za uongozi, yeye daima alibaki kuwa mwenye tabasamu lisilo na kikomo kwa huduma za wagonjwa na wasio na makazi na katika kufundisha katekisimu kwa watoto na vijana. Licha ya kupungikiwa na nguvu za kimwili, bado alitolea muda wake mwingi katika sala. Mwonekane wake unawaweza kufananishwa na wanatafakari wakuu wa sala; uwepo wake wa kila wakati mbele ya Ekaristi takatifu, akiwa na rosari mkononi na macho yakitazama msalaba, aliweza hapo kutafakari Mateso ya Yesu akiunganisha na hisia za Maria, mwenye upendo uliojaa uchaji unaojulikana kwa jina la Bikira wa mateso.

Tarehe 14 Mei 1940, kwa utlivu mkubwa kabisa, aliaga dunia.

Madre Rosa D’Ovidio

Mama Rosa D;Ovidio alizaliwa kule Lanciano tarehe 27 Juni 1857, wazazi wake ni Pasquale na Angelika Salvadori. Familia ya D’Ovidio iliishi katika maeneo ya Civitanova na ilijihusisha sana na maisha ya ukristu. Baba yake alijihusisha na biashara ya mimea ya kutengezea kamba akisaidiwa na jamaa zake wanapokuwa huru na shughuli za kifamilia zao.

Alipokuwa na miaka 29 alijiunga na umoja wa Chama cha wito, aliweka nadhiri zake za muda tarehe 6 Januari 1888 na hivyo aliteuliwa mapema kujiunga na jumuia ya Roma.

Mwaka 1892 aliteuliwa kuwa Mama mkubwa wa nyumba ya Roma. Huku akitiwa moyo na viongozi waandamizi wa Kanisa, hapo disemba 1896 yeye pamoja na masista wengine waliondoka kwa ajili ya kufungua utume mpya huko Pola, mahali ambapo walikaribishwa vizuri kwani katika mji huo hapakuwepo mashirika mengine ya kitawa ya wanawake. Askofu wa jimbo hilo alikuwa na uhusiano mzuri sana nae, hata alisifia roho yake nzuri, busara ya utendaji, ubunifu, ushujaa hasa utambuzi wa wajibu halisi ndani ya Shirika. Kwa njia ya msaada, ushupavu na uwajibikaji wa masista, ulipelekea kukamilika kwa ujenzi wa nyumba ya Mioyo Mitakatifu ikianzia na nyumba ya malazi halafu ya yatima na kikanisa jirani kilichowekwa chini ya usimamizi wa Moyo wa Yesu. Kwa maisha yake yote alitumia muda wa utendaji wake wa kazi huko Pola; alitumia nguvu zake zote kwa kazi mbali mbali mpya na pia ujenzi wa nyumba katika miji jirani. Wakati nguvu zake za kimwili zilipopungua, hakuruhusiwa kufanya tena kazi za kitume bali alipelekwa kuishi huko Cherso kwenye nyumba ya wazee iliyoitwa ‘Seppi’, mahali ambapo masista walikuwa wakitoa huduma kwa wazee. Alitumia muda mwingi katika sala za kina na huduma ndogo ndogo.

Akisaidiwa na masista wenzake, mnamo tarehe 27 Februari 1930, alifariki kwa utulivu wote.

Utendaji wao, iwe wakati wa mwanga au wa giza, umekuwa chachu ya uhai katika kukuza utakatifu wa kila moja binafsi na wa Shirika. Wakidumu  kila wakati na muunganiko na Yesu na Maria kama taa yao, wamejikuta wanadumu daima kwa mwenendo wa dhati uliowafanya watambue mapenzi ya Mungu kwa njia ya unyenyekevu wa ndani na utii kwa Kanisa.