Shirika

Wamisionari wa Mioyo Mitakatifu ya Yesu na Maria wameitwa ili kutoa ushuhuda wa upendo wa Mungu kwa watu, kwa njia ya kazi mbali mbali za kitume na huduma za upendo.

Waanzilishi wetu Rosa Rosato na Rosa D’Ovidio kwa njia ya vipaji vyao na juhudu zao binafsi walibuni na kuunda karama ya shirika ile ambayo toka kwayo twawezeshwa kuuishi ufuasi wa Moyo wa Yesu, kwa njia ya mwanga wa Moyo wa Maria, kwa madhumuni ya kuwasaidia ndugu zetu masikini na wanaoteseka.


 YUU YETU


Juhuda yao ya upendo na kujitoa sadaka imepata kuigwa na watu wengi, ambao kwa muda mfupi wa karne mmoja ya maisha, wameacha kumbukumbu ya dhati na ya kihistoria kwa Kanisa na kwa nyakati hizi.

Familia yetu ya Kitawa, kwa hakika, imekuwa ikijihusisha na mazingiza mbali mbali,  kwani imedhihirisha katika muda mfupi uliopita na hata leo ule uaminifu wake kwa Mungu na kwa binadamu kwa njia ya ushuhuda wa Kikristo na wa utendaji ulio hai.

Mwaka 1963 ulianzishwa utume wa shirika wa kwanza wa kimisionari huko Brazili.


 HISTORIA


Katika kipindi cha sehemu ya pili ya karne ya 19 Kanisa lilikuwa na msisitizo wa pekee kwa Moyo wa Yesu, ambao ni kielelezo cha upendo wa  ndani wa Mungu Baba kwa wanadamu.

Ibada ya uchaji kwa Moyo wa kimungu wa Yesu ilisisitizwa sana na Mapapa kwa Kanisa zima, kwani ikawa na mguso wa pekee kwa  Mama zetu Rosa Rosato na Rosa D’Ovidio katika kung’amua huruma kwa Moyo wa Yesu, ambayo tayari ilistawishwa na kuwa sehemu ya maisha yao tangu awali.

Papa Leo XIII hapo mwaka 1886 aliwapokea kwa upendo wa kibaba na kuwakabidhi kwa Vika wake. Wao waliunda makazi yao ya awali pale Mtaa wa Sagrestia namba 10 hukoVatikani.

Kazi yao ya kwanza ya utume nje ya nyumba ilikuwa kutembelea wagonjwa na wasio na makazi; na hapo ndipo palipojitokeza nafasi ya kutumia nguvu zao na maono yao katika kuufanya Upendo wa Mioyo ya Yesu na Maria vijulikan na kutangaza upendo wa kujitoa sadaka kwa ajili ya wokovu wa roho za watu.

Tangu mwaka 1887 kwa ongezeko la wanachama, utume wetu ulienea Italia yote.

Mnamo Disemba 1896 kwa mwaliko wa Vika Kardinali, Mama Rosa D’Ovidio pamoja na masista wengine walianzisha jumuia ya kwanza nje ya mipaka yetu huko Pola (Istria-Austria).

Baada ya maisha yaliyojaa uchaji wa kiroho na utume Mama Rosa D’Ovidio alifia huko Cherso mwaka 1930 na Mama Rosa Rosata alifia Roma mwaka 1940, wakiwa wameliachia Shirika urithi wa fadhili za unyenyekevu na utii.

Mwaka 1975 kwa njia ya ‘Hati ya Sifa’, Shirika la Kitawa la Mioyo Mitakatifu lilipata Hadhi ya Kipapa na likaongezewa jina la wasifu wake – Wamisionari – na hivyo kuongeza uanzilishwaji wake kwinginepo; Korea mwaka 1989; Tanzania mwaka 2000; na Guatemala mwaka 2005.


 WAANZILISHI WA SHIRIKA


Mnamo mwaka 1885 Rosa Rosato na mwaka 1888 Rosa D’Ovidio wakiwa tayari wameweka nadhiri zao za muda walijiunga na chama cha “watumishi wadogo wa Mioyo Mitakatifu’ huko Lanciano, Chieti kilichokuwa na idhini ya askofu wa mahali hapo.

Mnamo Februari 1886 Sista Rosa Rosato pamoja na masista wengine walitumwa kwenda huko Roma, kwa lengo la kufungua nyumba ndogo ya Shirika; walipoenda huko kwanza awali walipanga chumba kimoja kilichokuwa na vifaa muhimu vya ndani.

Wakiwa na tahadhari, wakuu wa Shirika walikwenda Roma kwa nia ya kuwatembelea masista na ndipo walimwomba na kumsihi Kardinali Vika ruhusa ya kufungua makao na kupangisha nyumba iliyokuwa Mtaa wa Sagrestia namba 10 kule Vatikano. Masista walianza kujihusisha na huduma kwa wagonjwa na wasio na mahali pa kuishi.

Mwaka 1888, Sista Rosa D’Ovidia aliitwa kwenda huko Roma pamoja na masista wengine. Mpaka wakati huu sista Rosa Rosato na sista Rosa D’Ovidio walijikuta wakifanya kazi kwa pamoja kwa faida ya wenye shida. Muungano wa Chama hicho, kwa ujumla, haukuweza hukudumu zaidi na hivyo ulitenganishwa na wakuu wa Kanisa. Jumuia ya Roma ilipewa uhuru kamili na hivyo kuibuka na kitu kipya cha aina yake kwa Kanisa na kujivika wajibu wa kuunda jumuia mpya ya kitawa kwa jina jipya la Masista wa Mioyo Mitakatifu ya Yesu na Maria.

Katika mwendelezo huo mpya, Mama Rosa Rosato na Rosa D’Ovidio walikuwa vyombo vya baraka ya Mungu, kwa njia ya kueneza ndani ya Kanisa zawadi ya Karama za pekee. Uelewa wa wajibu huu ulijitokeza ndani mwao hata kama kila moja kwa jinsi yake.