Picha

Utangulizi: Sista Maria Lidia Rosmarino – Mama Mkuu

Mnamo Julai 2015, baada ya kusubiri kwa muda mrefu tena kwa hamu kubwa kazi ngumu na ya utafiti, hatimaye tumepokea mikononi  mwetu sehemu ya kwanza ya historia na maisha ya  Waanzilishi wetu ambao huko nyuma kila mmoja alitazamwa peke yake. Tuliona kuwa ni muhimu kufafanua historia ilyoenea na kujulikana ya hawa waanzilishi wetu kwa ajili ya wavulana, wasichana na vijana. Kwa hiyo tuliamua kukabidhi kazi hii kwa Padre Massimiliano Taroni, mwandishi wa habari wa Kifransiskani ambaye kwa muhtasari aliunganisha maisha ya waanzilishi hawa wawili katika historia moja. Lugha iliyotumika kusimulia na kuelezea itasaidia wasomaji kufaidika na ushuhuda wao wa maisha.

Tunapoangalia maelezo ya historia ya maisha ya Mama Rosa Rosato na Mama Rosa D’Ovidio, tunashangazwa na ukweli kwamba licha ya mapungufu yao, walikuwa wazi kwa tendo la neema ya Mungu na kwa moyo ulio tayari wakajitoa na kuwa vyombo vya kazi za kustaajabisha. Udhaifu unadhihirisha hasa kuwa wokovu unatoka kwa Bwana na kwamba Yeye hukamilisha udhaifu huo pale unapokabidhiwa Kwake kwa imani na uvumilivu. Roho Mtakatifu alifanya kazi ndani yao na kuwaponya majeraha makubwa akiyafanya maumivu yao kuwa shukrani na msamaha; kwa hiyo, kutokana na tunu walizozipokea wakaanzisha familia ya shirika letu.

Historia hii fupi ya waanzilishi wetu inatusaidia kujifunza undani na unyenyekevu aliouishi Mama Rosa Rosato na ujasiri na ubunifu ulioonyeshwa na Mama Rosa D’Ovidio.

Mfano wao kwetu sisi wote uwe kichocheo cha kuishi maisha ya wakfu kwa shauku na bidii ilele walioyokuwa nayo wao licha ya magumu yasiyoepukika tunayokutana nayo ambayo daima huambatana na kazi za Mungu.

Massimiliano Taroni ni Padre wa Shirika la Ndugu Wadogo Wafransiskani. Alipewa Daraja ya Upadre mwaka 1992 na kuanza kuwa Mwandishi mwaka 1993. Kwa miaka kumi na miwili amekuwa Paroko Msaidizi katika parokia iliyo nje ya jiji la Milano na Mkurugenzi wa Malezi ya Vijana. Kwa miaka kumi na miwili amekuwa akifanya kazi kama mhamasishaji wa kimisionari na kiongozi wa misioni za kifransiskani katika nchi mbalimbali ulimwenguni kote. Kwa miaka mitano amesimamia gazeti la kimisionari na kuweza kuchapisha mamia ya kazi: majarida 65 yanayohusu maisha ya watakatifu na mashahidi wa imani, na vitabu kadhaa vinavyohusu ibada ya Moyo Mtakatifu na vitu vingine vya msaada kwa ajili ya Katekesi ya kuingizwa katika Ukristo.


Karama iliyozaliwa katika ufuasi” Sheria au kupakua >>


Utangulizi: Sista Maria Lidia Rosmarino – Mama Mkuu

Mtukuka Sista Tarsilla Osti ambaye ni mhusika wa simulizi hili anastaajabisha kwa upendo wake mkubwa kwa Yesu Msulibiwa na kwa Ekaristi; upendo uliojidhihirisha katika hali halisi ya maisha ya kila siku, hasa katika kuhudumia wagonjwa.

Yeye hakufanya mambo makubwa, lakini alifanya kuwa makubwa matendo madogo ya kila siku kwa vile alifanya yote akisukumwa na upendo na nguvu ya ndani iliyomfanya kustahimili kwa furaha kila aina ya sadaka na matatizo.

Alikuwa mtawa mnyenyekevu aliyekuwa tayari kabisa kupokea neema ya Mungu ambayo ilimfanya daima akue kiroho kwa undani zaidi na daima kujitahidi kutimiza mapenzi ya Mungu na imani isiyo na ukomo katika sala.

Baada ya kuchapisha kijitabu hiki, ninawatakia wasomaji, kwa msaada wa neema ya Mungu, waweze kufahamu utajiri wa maisha ya ndani ya Mtukuka na kuwa lishe kwa wenye hamu ya kuiga fadhila zake.

 

Padre Massimiliano Taroni ni wa Shirika la Ndugu Wadogo Wafransiskani. Alipewa Daraja ya Upadre mwaka 1992 na kuanza kuwa Mwandishi mwaka 1993. Kwa miaka kumi na miwili amekuwa Paroko Msaidizi katika parokia iliyo nje ya jiji la Milano na Mkurugenzi wa Malezi ya Vijana. Kwa miaka kumi na miwili amekuwa akifanya kazi kama mhamasishaji wa kimisionari na kiongozi wa misioni za kifransiskani katika nchi mbalimbali ulimwenguni kote. Kwa miaka mitano amesimamia gazeti la kimisionari na kuweza kuchapisha mamia ya kazi: majarida 65 yanayohusu maisha ya watakatifu na mashahidi wa imani, na vitabu kadhaa vinavyohusu ibada ya Moyo Mtakatifu na vitu vingine vya msaada kwa ajili ya Katekesi ya kuingizwa katika Ukristo.

Mtukuka Sista Tarsilla Osti – Moyo wa Kiekaristi” Sheria au kupakua >>